Top Ad unit 728 × 90

‘SINTAH’ AMPA POLE ‘JACKLINE WOLPER’, AMTAKA KUYAKUMBUKA MAGARI YAKE YA ZAMANI…. NI BAADA YA KUACHWA NA ‘DALLAS’…!!

WAKATI hali ya kimaisha ikiwa tete kwa msanii anayefunika kwa urembo bongo movie Jackline Wolper, ambaye alikuwa akitembelea magari ya kifahari kila kukicha, sasa anachoambulia ni pole kwani shosti yake wa karibu Sintah, amedai kuwa kuachana kwao na ‘Dallas’ kutamfanya Wolper ayakumbuke magari yake ya zamani kama vile Noah.

Wolper ni msanii wa kwanza bongo kutembelea magari ya kifahari tena baada ya kumpata jamaa huyo lakini awali kabisa alikuwa akitembelea Noah, na inadaiwa kuwa sasa atakuwa akiyaona kwa macho watu wakiendesha kwani Dallas amechukua funguo zote za magari yake.

Ishu hii ikiwa inashika kasi mjini huku watu wakiwa macho juu kutaka kuona nini kinachoendelea kwa Wolper, Sintah hakusita kudai kuwa mara nyingi mapenzi ya kwenye magazeti huwa hayadumu kwani awali kabisa Wolper alijitangazia kuwa hawawezi kuachana na Dallas huku akisahau kuwa kuna wabaya wake wanaomtazama.

Sinta alidai kuwa kwa jinsi anavyomfahamu Wolper haoni kama yeye atakuwa ndiye chanzo cha kuachana kwao kwani kuna wabaya wake ambao wamejaa fitna, lakini kwa upande wake anampa pole ili sasa ajipange na kuacha tabia ya kuishi mjini kwa kuwatengemea wanaume, hasa wale anaokutana nao mjini.

“Kuachana ni kawaida miaka ya sasa kwanza kama huna hela huwezi kutembea na staa bongo na Dallas alimpenda Wolper kwa sababu ni staa, lakini sioni kama kuna tatizo wao kuachana kwani wamekutana mjini na wanaachana kimjini,” alidai.

Mwandishi wa habari hizi bila shaka alitaka kuzungumza na Wolper ili kujua kama ataanza kutembelea gari lake la zamani Noah, lakini alipopokea simu alidai yuko bize na kazi za kifamilia hivyo hawezi kuzungumza lolote ingawa swali lilikuwa ni dogo ambalo halikuwahitaji dakika hata mbili kulijibu.

‘SINTAH’ AMPA POLE ‘JACKLINE WOLPER’, AMTAKA KUYAKUMBUKA MAGARI YAKE YA ZAMANI…. NI BAADA YA KUACHWA NA ‘DALLAS’…!! Reviewed by Unknown on Wednesday, October 03, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.